Kama ukipendelea, kuna nakala ya kiingereza.
Mtumiaji hatafunguliwa akaunti ya kutumia kompyuta (Jina la mtumiaji, Jina la mficho) na huenda hatatumia kabisa kompyuta za chuo hadi atakapokubaliana na mambo yafuatayo:
Watumiaji wote wa Kompyuta (wafanyakazi, wakufunzi, na wengineo) Wanatarajiwa kuwajibika kwa mienendo yao katika mfumo mzima wa kompyuta pamoja na Mtandao kama wanavyokuwa mahali pengine chuoni. Watumiaji wanakumbushwa kuwa matendo yao yanaweza kuwakilisha jumuia nzima ya chuo. Kwa mfano uteuzi wa mambo wanayoangalia kwenye mtandao, lugha wanayotumia, mawazo wanayotoa na mengine yote wanayoyafanya. Watumiaji wa kompyuta wanatakiwa kujua kuwa yote wanayofanya katika chumba cha kompyuta yanafuatiliwa.
Watumiaji wa Kompyuta wanapaswa kuzingatia sheria/kanuni na taratibu zilizowekwa ikiwa ni pamoja na hizi: Sheria zimebandikwa ndani ya maabara ya kompyuta na katika mtandao (LAN) wa chuo ambazo zinaweza kubadilika kulingana na wakati. Watumiaji wanawajibika kuzifahamu/kuzielewa sheria zote ikiwa na pamoja na sheria mpya zitakazotolewa na uongozi wa chuo.
Kama huna uhakika wa nini cha kufanya kama vile kuletewa ujumbe wa kukosea Mtandao. Ujumbe usioufahamu/usioeleweka, kuharibika kwa kifaa cha kompyuta, na Muulize msimamizi wa maabara ya kompyuta. Heri kusubiri na kuuliza kuliko kufanya jambo/kitendo kitakachokuhatarisha wewe binafsi, kompyuta na mtandao mzima.
Kukiukwa kwa Sheria Yeyote Hapo Juu kunaweza kusababisha yafuatayo: |
Nimesoma mkataba huu na kuzingatia yote yaliyotajwa hapo juu.
Sahihi: | ||
Jina: | ||
Tarehe: |
Jina la Mtumiaji | Jina la Mficho |
25-Jul-2007 | Damari Mchome | Corrections |
14-May-2007 | Damari Mchome | Translate to Kiswahili |
14-Feb-2007 | Albert Lingelbach | Re-formulation from source document |
Kleruu Teachers College | Original version |